Luke 3:4-6

4 aKama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu aliaye nyikani,
‘Itengenezeni njia ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.

5 Kila bonde litajazwa,
kila mlima na kilima vitashushwa.
Njia zilizopinda zitanyooshwa,
na zilizoparuza zitasawazishwa.

6 bNao watu wote watauona
wokovu wa Mungu.’ ”

Copyright information for SwhKC